Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2015

MSIMAMO LIGI KUU UINGEREZA

Picha
MSIMAMO LIGI KUU UINGEREZA 

RATIBA LIGI KUU UINGEREZA WIKI HII

Picha
  Katika ligi kuu uingereza wiki hii mechi zitachezwa katika wiwanja mbalimbali na mechi kubwa ambayo inavuta hisia za wengi ni ile kati ya Tottenham Hotspur na Manchester city, lakini tukiachana na hiyo pia mashabiki wa soka leo wanatarajia kuona kama Leceister wataendeleza ubabe wao wa kuto kupoteza mechi kwani mpaka sasa ni wao pekee ambao hawajafungwa na wanashika nafasi ya 4 mbele ya mpinzani wao wa leo Arsenal ambaye anashika nafasi ya tano akiwa na pointi 10

RATIBA LIGI KUU BARA

Picha
  Katika mwendelezo wa ligi kuu Tanzania bara leo watani wa jadi Simba na Yanga wanakutana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ikiwa kila timu inakamilisha mechi yake ya nne tangu kuanza kwa ligi msimu huu wa 2015/16.Mechi hii inatarajiwa kuanza majira ya saa 10:00 jioni. Mechi nyingine za Ligi Kuu ya Vodacom leo zitakuwa ni kati ya Coastal Union dhidi ya Mwadui FC katika Uwanja wa Mkwakwani mijini Tanga, Prisons na Mgambo JKT Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, JKT Ruvu na Stand United Uwanja wa Karume, Dar es salaam, Mtibwa Sugar na Majimjaji ya Songea Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro na Kagera Sugar na Toto Africans Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo miwili, kati ya Azam FC na Mbeya City Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na African Sports na Ndanda FC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

RAIS WA FIFA SEPP BLATTER ACHUNGUZWA

Picha
Rais wa shirikisho la soka duniani Fifa Sepp Blatter anachunguzwa na viongozi wa mashtaka nchini Uswizi. Afisi ya mwanasheria mkuu wa serikali imesema Blatter anachunguzwa kwa “tuhuma za kuhusia katika usimamizi mbaya pamoja na – labda – tuhuma za kutumia vibaya pesa”. Bw Blatter amehojiwa na pia afisi yake ikapekuliwa, Ofisi hiyo imesema. Uchunguzi huo unahusu mkataba wa haki za utangazaji wa runinga ambao Blatter alitia saini pamoja na aliyekuwa mkuu wa soka wa eneo la Caribbea Jack Warner mwaka 2005. Bw Blatter pia anatuhumiwa kufanya “malipo yasiyo halali” mwaka 2011 kwa rais wa shirikisho la soka Ulaya Uefa Michel Platini, taarifa ya afisi hiyo imesema. Mwezi Mei, maafisa saba wakuu wa Fifa walikamatwa Zurich kwa tuhuma za ufisadi kutoka kwa maafisa wa mashtaka nchini Marekani. Blatter alishinda uchaguzi wa urais wa Fifa mara ya tano mfululizo Mei 29 lakini, baada ya tuhuma za ufisadi kukumba shirikisho hilo, alitangaza Juni 2 kwamba angejiuzulu. Anatarajiwa kuondoka wadhifa wa...

SIMBA VS YANGA HAPATOSHI TAIFA LEO

Picha
WATANI wa jadi, Simba na Yanga SC wote walirejea jana Dar es Salaam kutoka kwenye kambi zao Zanzibar kuelekea pambano lao la leo. Miamba hiyo inatarajiwa kumenyana leo jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuanzia Saa 10:00.

KICHAPO CHA BARCA CHALETA HESHIMA LA LIGA

Picha
Barcelona walipokezwa kichapo chao kikubwa zaidi La Liga wakiwa chini ya Luis Enrique baada ya kulazwa 4-1 na Celta Vigo Jumatano.

CHELSEA KUMSAJILI BEKI WA BARCA

Picha
Chelsea wapo kwenye harakati za kumsajili beki  wa Barcelona Dani Alves ili kuweza kuboresha safu yao ya ulinzi,taarifa kutoka kwa vyombo vya habari vya Hispania.

RATIBA EPL (CHELSEA, ARSENAL USOKWA USO)

Picha
Mechi katika viwanja mbalimbali wiki hii zitaendelea huku katika ligi ya Uingereza ambapo siku ya kesho takribani viwanja 7 nyasi zitakuwa zikiwaka moto mpambano mkubwa unaosubiliwa kwa hamu ni ule wa mabingwa watetezi wa ligi hiyo Chelsea na watani wao wa jadi Arsenal

CHELSEA YASHINDA,ARSENAL YACHAPWA UEFA

Picha
Timu ya soka ya Arsenal ikicheza ugenini imekubali kuchapwa 2-1 na timu ya Dinamo Zagreb katika mchezo wa klabu bingwa barani ulaya, Oxlade-Chamberlain alianza kujifunga kisha Junior Fernandes huku bao la Arsenal likifungwa na Theo Walcot.

DAVID DEGEA TAYARI KURUDI KIKOSINI

Picha
David De Gea alianza katika mchezo wa Hispania dhidi ya Macedonia

MWANA WA MFALME AJITOSA TENA URAIS FIFA

Picha
Mwanamfalme wa Jordan Ali Bin Al-Hussain ametangaza kuwa atasimama kuwania nafasi ya Urasi wa Shirikisho la kandanda duniani FIFA kurithi nafasi ya Rais wa sasa anayestaafu Sepp Blatter.

KUCHEZA JUMAMOSI KWAZUA MVUTANO ISRAEL(PICHA)

Picha
Mamlaka ya soka nchini Israel imesimamisha mipango ya mgomo katika mzozo kuhusu kucheza siku ya Sabato ya Wayahudi.

USAJILI WA MAN UTD KWA MWAKA 2015/16

Picha
  Hawa ndio wachezaji waliosajiliwa na klabu ya Manchester United katika majira haya ya kiangazi kwa msimu wa mwaka 2015/16,wachezaji walikotoka ikiwa ni pamoja na gharama zao na malipo yake

MJUE JAMES RODRIGUEZ

Picha
 Jina kamili anaitwa James Rodriguez akiwa na takribani miaka 24, alizaliwa Jul 12, 1991 katika mji wa   Cúcuta nchini Colombia , urefu wake ni mita 1,80 m, kwa sasa ni mchezaji wa klabu ya Real Madrid inayoshiriki ligi kuu ya Hispania alimaarufu kama Laliga.Rodriguez alijiunga na klabu hiyo Jul 22, mwaka 2014 kwa ada ya uhamisho wa Euro 80m.

RODRIGUEZ AUMIA

Picha
Real Madrid imejawa na hfu juu ya uimara wa kiungo wao mshambuliaji James Rodriguez baada ya kiungo huyo kuumia kifundo cha mguu(enga) wakati akicheza mchezo wa kimataifa wa taifa lake la Colombia.

SCHWEINSTEIGER AIGHARIMU MAN UTD EURO 6.5m TU!

Picha
Bastian Schweinsteiger’s boyhood club, TSV 1860 Rosenheim, wameweka wazi kuwa Manchester United imeilipa Bayern Munich £6.5m tu kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujeruman wakati huu wa kiangazi.

JUAN MATA AING'ARISHA HISPANIA KUFUZU EURO 2016

Picha
Kiungo wa Barcelona, Sergio Busquets akimpongeza Juan Mata (kushoto) baada ya krosi yake kuipa bao pekee la ushindi Hispania dhidi ya Macedonia mchezo wa Kundi C kufuzu Euro 2016 mjini Skopje.

SIMBA, YANGA WACHEZAJI NA MAKOCHA WOTE WAPEWA BIMA BURE TIMU ZOTE LIGI NZIMA

Picha
  MFUKO wa Bima ya Afya nchini (NHIF) umeingia makubaliano ya udhamini wa bima ya afya kwa wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi kwa klabu 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kipindi cha mwaka mmoja

YANGA SC WAWEKA KAMBI KUJIANDAA NA WAGOSI WA KAYA

Picha
MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga SC jana wameingia kambini katika hoteli ya Valley View, Mtaa wa Kongo, Kariakoo, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wao wa kwanza wa LIgi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union Jumapili.

SERENA WILLIAM AMSHINDA DADA YAKE US OPEN

Picha
Serena williams amemshinda dada yake Venus william katika mashindano ya US Open na kuzidi kusonga mbele katika ushindi mara mbili wa kalenda ya kwanza ya Grand Slam.

ROONEY AVUNJA REKODI YA SIR BOBBY

Picha
Wayne Rooney ameivunja rekodi ya upachikaji mabao ya muda wote katika timu ya taifa ya England, iliyokuwa ikishikiliwa na Sir Bobby Charlton katika mchezo dhidi ya Switzerland,uliopigwa uwanjani

HANS POPPE AMTAKA MALINZI AWAADABISHE VIONGOZI YANGA WANAOTAKA KUVURUGA AMANI TAIFA STARS

Picha
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amemtaka Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwachukulia hatua viongozi wa Yanga SC wanaotoa kauli za uchochezi kuhusu timu ya taifa.

UFARANSA YAICHAPA 2-1 SERBIA

Picha
Mshambuliaji wa Ufaransa, Olivier Giroud akimiliki mpira mbele ya beki wa Serbia, Ivan Obradovic katika ushindi wa 2-1 jana kwenye mchezo wa kirafiki.

LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA MLANGONI

Picha
RATIBA YA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA Septemba 12, 2015 Ndanda FC Vs Mgambo JKT African Sports Vs Simba SC Majimaji FC Vs JKT Ruvu Azam FC Vs Prisons

MKUTANO MKUU TFF KUFANYIKA DESEMBA 10 NA 20

Picha
KIKAO cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kilichokafanyia Septemba 6 mwaka huu kimepanga tarehe ya Mkutano Mkuu wa shiriisho hilo.

UJERUMAN YAPIGA MTU 3-2 EURO

Picha
  Ujerumani imeitandika 3-2, Scotland ikiwa nyumbani kwao katika uwanja wa Hampden Park kwenye mechi ya kufuzu Euro 2016 iliyofanyika usiku wa kuamkia leo.

AND MURRAY NJE US OPEN

Picha
Mcheza Tenisi Andy Murray ameyaaga mashindano ya US Open baada ya kuchapwa na Kevin Anderson wa Afrika ya kusini.

UHOLANZI YAPIGWA 3-0 NA UTURUKI

Picha
Uturuki imeshinda 3-0 mabao ya Oguzhan Ozyakup dakika ya nane, Arda Turan dakika ya 26 na Burak Yilmaz dakika kabla ya filimbi ya mwisho.

MWINGEREZA SIMBA AKOMAA NA NGOZI

Picha
KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Muingereza, Dylan Kerr, amesema kwamba kikosi chake kimepanga kufanya vizuri katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ambayo inatarajiwa kuanza Jumamosi kwa kupata ushindi wa 'kihistoria' ugenini itakapokabiliana na wenyeji African Sports kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini, Tanga.

MKWASA KUPATA ULAJI WA KUDUMU STARS

Picha
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) lipo katika mchakato wa kumpa Mkataba wa kudumu, kocha wa muda wa timu ya taifa, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa. Pamoja na kucheza mechi tatu bila kushinda, lakini TFF imeridhishwa na maendeleo ya timu kutoka ilivyokuwa chini ya kocha Mholanzi, Mart Nooij na imeshawishika kumpa Mkataba wa kudumu Mkwasa.

YANGA SC WAIENDEA BAGAMOYO COASTAL UNION, PATACHIMBIKA TAIFA JUMAPILI

Picha
MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga SC Jumatano wataingia kambini katika hoteli ya Kiromo, Bagamoyo mkoani Pwani kwa maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom mwishoni mwa wiki.

MURRAY ATINGA 16 BORA US OPEN (PICHA)

Picha
Andy Murray atinga hatua ya 16 bora kwa kumfunga Thomaz Bellucci katika michuano ya US open inayoendelea nchini Marekani. Muingereza Andy Murray amepata mafanikio mepesi katika michuano ya US Open mnamo raundi ya nne baada ya kumcharaza mfululizo Mbrazili Thomaz Bellucci.

MATOKEO YA KUFUZU AFCON 2017 HAYA HAPA

Picha
  Algeria ilifunga kwa mara ya pili katika dakika ya tano za mwisho na kusajili ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya Lesotho katika michuano ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2017. Faouzi Ghoulam alifikisha Algeria katika ngazi ya juu katika dakika ya 31 lakini baada ya dakika sita wenyeji wakafunga bao la kusawazisha kupitia kwa Ralekoti Mokhahlane.

UJERUMANI,SERBIA ZANG'ARA EUROPA(MATOKEO YA MECHI ZOTE HAYA HAPA)

Picha
Timu ya taifa ya Ujerumani imepanda hadi kileleni mwa msimamo wa kundi D la michuano ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya barani Ulaya mwaka 2016 baada ya kuichabanga Poland magoli 3 - 1. Thomas Muller ndiye aliyefungua

BALE AWAJAZA FURAHA WALES

Picha
Meneja wa timu ya taifa ya kandanda ya Wales Chris Coleman amewahimiza mashabiki wakubali “kutekwa na furaha ya ufanisi” lakini akasema wachezaji wake hawatafanya hivyo hadi wafuzu kwa Euro 2016. Baada ya kucharaza Cyprus 1-0 Alhamisi, Wales watafuzu wakiandikisha ushindi dhidi ya Israel Jumapili.

IOC KUFADHILI MICHEZO YA WAKIMBIZI

Picha
Shirikisho la michezo ya Olimpiki, IOC, leo limetangaza hazina ya dola millioni mbili, ambazo zitatolewa kwa Kamati ya Kitaifa ya olimpiki ya nchi wanachama kufadhili miradi itakayowasaidia wakimbizi katika mataifa yao. Rais wa IOC, Thomas Bach, amesema kuwa kama shirikisho la

MAN UTD MTIHANI KATIKA USAJILI

Picha
Rais wa kilabu ya Real Madrid amesema Manchester United hawana uzoefu kuhusu kuhama kwa wachezaji na ndiyo sababu uhamisho wa David De Gea ulitibuka. Florentino Perez aligusia pia kushindwa kwa United kusajili Fabio Coentrao kutoka Real na Ander Herrera wa Athletic Bilbao siku

WELBECK NJE MPAKA DISEMBA

Picha
  Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Danny Welbeck atakuwa nje ya Uwanja mpaka mwezi Disemba baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye Goti . Arsenal imeeleza kuwa matibabu kwenye Goti hilo hayakwenda vizuri na Wiki iliyopita ikaamuliwa afanyiwe operesheni.

ARGENTINA VINARA KWA UBORA DUNIANI

Picha
  Shirikisho la Soka duniani Fifa imetoa orodha ya Ubora Duniani kwa mwezi wa Nane ambapo Argentina inaongoza ikiwa nafasi ya kwanza. Ubelgiji wao wako katika nafasi ya pili huku mabingwa wa dunia Ujerumani wakiwa katia nafasi ya tatu.

SIMBA YA KAMILIKA

Picha
SIMBA SC imesajili wachezaji 27 kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara unaoanza wiki ijayo. Katika orodha hiyo, Simba SC imekamilisha orodha ya wachezaji saba wa kigeni kwa kuwasajili Vincent De Paul Angban wa Ivory Coast, Emery

MAN UTD TUMBO JOTO KWA MARTIAL

Picha
Anthony Martial ataweza akaigharimu klabu ya Manchester United £57.6m kama malipo hayatafanyika mapema. Makamu wa Rais wa Monaco Vadim Vasilyev ameitahadharisha Manchester United kwamba huenda ikawa ni mara tatu ya malipo ofa ya Anthony Martial ndani ya wiki, na akathibitisha kuwa uhamisho wa mchezaji huyo unakaribia £58m.

PAPY AACHWA NA CHELSEA UEFA

Picha
Mchezaji aliyesajiliwa hivi majuzi na Chelsea, Papy Djilobodji, ameachwa nje ya kikosi cha klabu hiyo kitakachocheza mechi ya ligi ya klabu bingwa Ulaya, hatua ya makundi.

DEGEA AKWAMA KUTUA REAL

Picha
Uhamisho wa Golikipa David De Gea kutoka Manchester United kwenda Real Madrid ya Hispania umekwama dakika za mwisho kwa sababu ya karatasi muhimu za uhamisho kuchelewa . Madrid walikua tayari kutoa dau la pauni milioni 29 , kipa wao Keylor Navas kama sehemu ya dili la uhamisho huo.