RATIBA LIGI KUU BARA

 
Katika mwendelezo wa ligi kuu Tanzania bara leo watani wa jadi Simba na Yanga wanakutana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ikiwa kila timu inakamilisha mechi yake ya nne tangu kuanza kwa ligi msimu huu wa 2015/16.Mechi hii inatarajiwa kuanza majira ya saa 10:00 jioni.
Mechi nyingine za Ligi Kuu ya Vodacom leo zitakuwa ni kati ya Coastal Union dhidi ya Mwadui FC katika Uwanja wa Mkwakwani mijini Tanga, Prisons na Mgambo JKT Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, JKT Ruvu na Stand United Uwanja wa Karume, Dar es salaam, Mtibwa Sugar na Majimjaji ya Songea Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro na Kagera Sugar na Toto Africans Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo miwili, kati ya Azam FC na Mbeya City Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na African Sports na Ndanda FC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii