Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya LIGI KUU

MSIMAMO LIGI KUU UINGEREZA

Picha
MSIMAMO LIGI KUU UINGEREZA 

RATIBA LIGI KUU BARA

Picha
  Katika mwendelezo wa ligi kuu Tanzania bara leo watani wa jadi Simba na Yanga wanakutana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ikiwa kila timu inakamilisha mechi yake ya nne tangu kuanza kwa ligi msimu huu wa 2015/16.Mechi hii inatarajiwa kuanza majira ya saa 10:00 jioni. Mechi nyingine za Ligi Kuu ya Vodacom leo zitakuwa ni kati ya Coastal Union dhidi ya Mwadui FC katika Uwanja wa Mkwakwani mijini Tanga, Prisons na Mgambo JKT Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, JKT Ruvu na Stand United Uwanja wa Karume, Dar es salaam, Mtibwa Sugar na Majimjaji ya Songea Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro na Kagera Sugar na Toto Africans Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo miwili, kati ya Azam FC na Mbeya City Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na African Sports na Ndanda FC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

SIMBA VS YANGA HAPATOSHI TAIFA LEO

Picha
WATANI wa jadi, Simba na Yanga SC wote walirejea jana Dar es Salaam kutoka kwenye kambi zao Zanzibar kuelekea pambano lao la leo. Miamba hiyo inatarajiwa kumenyana leo jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuanzia Saa 10:00.

YANGA SC WAWEKA KAMBI KUJIANDAA NA WAGOSI WA KAYA

Picha
MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga SC jana wameingia kambini katika hoteli ya Valley View, Mtaa wa Kongo, Kariakoo, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wao wa kwanza wa LIgi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union Jumapili.

MWINGEREZA SIMBA AKOMAA NA NGOZI

Picha
KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Muingereza, Dylan Kerr, amesema kwamba kikosi chake kimepanga kufanya vizuri katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ambayo inatarajiwa kuanza Jumamosi kwa kupata ushindi wa 'kihistoria' ugenini itakapokabiliana na wenyeji African Sports kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini, Tanga.