MATOKEO YA KUFUZU AFCON 2017 HAYA HAPA

 Image result for MATOKEO AFCON 2017
Algeria ilifunga kwa mara ya pili katika dakika ya tano za mwisho na kusajili ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya Lesotho katika michuano ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2017.
Faouzi Ghoulam alifikisha Algeria katika ngazi ya juu katika dakika ya 31 lakini baada ya dakika sita wenyeji wakafunga bao la kusawazisha kupitia kwa Ralekoti Mokhahlane.

Image result for MATOKEO AFCON 2017
Wachezaji wa Algeria wakishangilia baada ya kufunga goli
Dakika ya 85 El-Arbi Hilal Soudan airudisha timu ya Algeria kifua mbele dakika chache kabla mchezo kukamilika.
Ushindi huo umerudisha Algeria juu ya jedwali katika kudi J huku Lesotho wakisalia mwisho bila alama yoyote.
Image result for MATOKEO AFCON 2017
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Chelsea ya Uingereza Mohamed Sallah akiwania mpira wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Misri kwenye mbio za kuwania kucheza fainali za Afcon 2017.
Mabingwa Ivory Coast walicheza mechi yao ya ufunguzi kwa kutoka sare na timu ya Sierra Leone.
Mechi hiyo ilichezwa katika uwanja wa Port Harcourt,Nigeria .
Sierra Leone bado wamepigwa marufuku ya kuwa wenyeji wa mechi za kimataifa kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Ilikuwa mwanzo mbaya kwa Michel Dussuyer tangu kung'atuka mamlakani kwa kocha wa Elephant's.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii