SIMBA, YANGA WACHEZAJI NA MAKOCHA WOTE WAPEWA BIMA BURE TIMU ZOTE LIGI NZIMA
MFUKO wa Bima ya Afya nchini (NHIF) umeingia makubaliano ya udhamini wa bima ya afya kwa wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi kwa klabu 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kipindi cha mwaka mmoja
Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano uliofnayika leo ofisi za TFF zilizopo Karume, Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine amesema wanaishukuru NHIF kwa kuwapa udhamini huo ambao utavisaidia vilabu vya Ligi Kuu katika matibabu ya wachezaji na bechi ka ufundi.
Tumekua na kilio cha muda mrefu juu ya vilabu vya Ligi Kuu kuwa na Bima za afya kwa wachezaji, kitu ambacho kipo kikanuni lakini vilabu vilikuwa vinashindwa kutimiza hitaji hilo la kikanuni na sasa TFF kwa kushirikian na NHIF tutakua tumeiondoa tatizo hilo.
Naye Mkuu wa Mawasiliano wa NHIF, Sungi amesema udhamini huo wa bima ya matibabu kwa wachezaji na benchi la ufundi utatolewa kwa matibabu yote yatakayofnayika ndani ya nchi.
Mchezaji au kiongozi pindi atakapopata tatizo la kuumwa, basi ataweza kutibiw akatika hospitali yoyote yenye huduma ya Bima katika eneo alilopo, lengo ni kuhakikisha wanakua na afya njema kwa ajili ya kushiriki vizuri mikikimikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom.
Lengo letu ni kuona wachezaji wanapata huduma ya afya popote wanapokuwa na kuweza kushiriki vizuri katika michuano ya Ligi Kuu, na kuweza kuzitumikia vyema timu zao kwenye mashindano.
Ofisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura kwa niaba ya vilabu vya Ligi Kuu amesema wanashukuru kupata udhamini huo wa bima ya afya, uwepo wa NHIF umevipunguzia vilabu mizigo wa matibabu na sasa vilabu vitaweza kushiriki vizuri kwenye michuano ya msimu huu.
TIMU ZA LIGI KUU
Timu zinazoshiriki Ligi Kuu ni Ndanda FC, Mgambo Shooting, African Sports, Simba SC, Majimaji FC, JKT Ruvu, Azam FC, Prisons, Stand United, Mtibwa Sugar, Toto Africans, Mwadui, Mbeya City, Kagera Sugar, Yanga SC na Coastal Union.
Maoni
Chapisha Maoni