WACHEZAJI

Nyota wa raga Johan Lomu aaga dunia
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Rugby Johan Lomu
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya New Zealand ya mchezo wa raga Johan Lomu amefariki dunia.Risala za rambirambi zimeendelea kutumwa kutoka kila pembe duniani.

Mchezaji huyu amefariki akiwa na umri wa miaka 40 huku akisumbuliwa na ugonjwa wa figo.

Lomu alifanyiwa uabadilishwaji wa figo yake, ambayo ilikua ikimsumbua, mwaka 2004 na iliyopelekea kustaafu kucheza mchezo wa raga.

Lomu enzi za uhai wake alichezea timu ya taifa michezo 73 kuanzia mwaka 1994 mpaka 2002 na kufunga mabao 43. Image copyright Getty

Anachukuliwa kama mmoja wa wachezaji nguli zaidi wa raga ya kimataifa.

Alifariki ghafla baada ya kurejea kutoka Uingereza ambako alikuwa ameenda kufanya kazi ya kupigia debe Kombe la Dunia la Raga lililomalizika majuzi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii