PAPY AACHWA NA CHELSEA UEFA

Mchezaji aliyesajiliwa hivi majuzi na Chelsea, Papy Djilobodji, ameachwa nje ya kikosi cha klabu hiyo kitakachocheza mechi ya ligi ya klabu bingwa Ulaya, hatua ya makundi.
Mlinzi huyo Djilobodji,mwenye umri wa miaka 26, kutoka Senegal, alisajiliwa na 'the Blues' siku ya mwisho ya kuhama wachezaji kutoka klabu ya Nantes ya Ufaransa kwa £4m.
Wachezaji wenzake waliojiunga majuzi na mabingwa hao wa Uingereza, Asmir Begovic, Abdul Rahman Baba, Pedro na Radamel Falcao wote wamejumuishwa kwenye kikosi hicho cha wachezaji 25.
Nyota huyo aliachwa nje kwa kuwa Chelsea, walikuwa tayari wamejaza nafasi za wachezaji ambao sio wazaliwa wa Uingereza kwenye kikosi chao cha kwanza.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii