KUMBUKUMBU
Jules Bianchi, 1989-2015: Ni dreva wa fomula 1(F1) ambaye wanamichezo hatuta msahau.
Kumbuka Jules Bianchi, ni dereva wa langalanga fomula one F1 ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 25,miezi tisa tu baada ya kupata ajali mwaka 2014 huko Japani,kamwe hawezi sahaulika...
Wakati Academi ya Ferrari mwaka 2010 ikiwatuma madereva wake, alikuwa ni Jules Bianchi ambaye walimchagua akiwa muwakilishi katika mashindano yaliyowahusisha Wafaransa na kuwaaminisha kuwa yeye ni dereva bora na wa ngazi ya juu akiwa na kipaji kilichogunduliwa na timu yake ya Maranello ya F1 ambayo ni maarufu na ndiyo iliyomlea pia.
Maisha yake yalikatishwa ghafla mara baada ya kupata ajali mbaya mwaka 2014 huko Japanese GP, kipaji cha Bianchi kilikuwa endelevu kwani kilionekana mapema tu pale alipoanza kuendesha magari yaendayo kwa kasi ambayo yalimtambulisha.
Bianchi
alizaliwa katika mji wa Nice kusini mwa Ufaransa mnamo tarehe 3 Agosti 1989. Familia yake tangu siku nyingi ilikuwa tayari inajihusisha na mashindano ya magari ya langa langa (motorsport) ambapo babu yake Jules, Mauro alisha wahi kuwa mbingwa wa dunia wa GT na mjomba wake mkubwa Lucien alishinda mwaka 1968 Le Mans kwa masaa 24 , pamoja na kianzio 17 Grands Prix.
Maoni
Chapisha Maoni