RODRIGUEZ AUMIA




Real Madrid imejawa na hfu juu ya uimara wa kiungo wao mshambuliaji James Rodriguez baada ya kiungo huyo kuumia kifundo cha mguu(enga) wakati akicheza mchezo wa kimataifa wa taifa lake la Colombia.Rodriguez 24, alifanyiwa mabadiliko wakati wa kipindi cha pili wakati Colombia ikienda sare ya 1-1 na Peru baada ya kubanwa kwa muda mrefu, lakini madaktari walimtoa kwa faida ya Madrid na kudai kuwa wamemtoa kwa tahadhari zaidi.

Ukiachana na taarifa ya madaktari hao Madrid wamesema watafanya uchunguzi wenyewe kwa mchezaji huyo na wanatumaini kuwa tatizo alilonalo ni dogo kutokana na hali yake tangu alipoanza msimu.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii