CHELSEA KUMSAJILI BEKI WA BARCA

Chelsea wapo kwenye harakati za kumsajili beki  wa Barcelona Dani Alves ili kuweza kuboresha safu yao ya ulinzi,taarifa kutoka kwa vyombo vya habari vya Hispania.
Mabingwa hao wa EPL wameweza kushinda mechi mbili tu kati ya sita walizocheza katika ligi msimu huu huku wakiwa wamefungwa jumla ya magoli.

Jose Mourinho pia alikaririwa akisema kuwa ameandaa £36.1m kwaajili ya a kumsajili beki wa kushoto wa  Valencia Jose Luis Gaya, lakini hali inaweza ikabadilika na nguvu nyingi kuelekezwa kwa Alves ambaye atagharimu kiasi kidogo cha  £14.5m.

Alves, mwenye umri wa miaka 32, amesaini miaka miwili tu kubakia kwenye timu yake ya sasa na wakati wa kiangazi mwakani anatarajiwa kuondoka.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii