TYSON KUZICHAPA NA KLITSCHKO
Klitschko na Tyson Fury wakirushiana makonde Pigano la marudio kati ya Tyson Fury na Wladmir Klitschko litaandaliwa mjini Manchester mnamo mwezi Julai tarehe 9 kulingana na mkufunzi wa bondia huyo wa Uingereza. Peter Fury alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter siku ya Ijumaa na tangazo jingine linatarajiwa baadaye.