IOC KUFADHILI MICHEZO YA WAKIMBIZI
Shirikisho la michezo ya Olimpiki,
IOC, leo limetangaza hazina ya dola millioni mbili, ambazo zitatolewa
kwa Kamati ya Kitaifa ya olimpiki ya nchi wanachama kufadhili miradi
itakayowasaidia wakimbizi katika mataifa yao.
Rais wa IOC, Thomas
Bach, amesema kuwa kama shirikisho la
michezo ya olimpiki, imehuzunishwa
na habari zainazowahusu wakimbizi, katika siku za hivi karibuni.
Amesema
IOC imekuwa ikifuatilia matukio yanayojiri katika eneo la Mashariki ya
Kati, Afrika na Ulaya na wao wanataka kutumia michezo kuwaleta wanainchi
pamoja, hasa kuwasaidia wakimbizi.
Amesema IOC imekuwa na
ushirikiano mwema na Umoja wa Mataifa na shirika lake linalowahudumia
wakimbizi UNHCR na watashirikiana kuhakikisha fedha hizi zimewanufaisha
wakimbizi na zaidi ya yote kujaribu kuleta amani na utengamano.
Kamati
za kitaifa za Olimpiki na mashirika mengine sasa zitahitajika kutuma
maombi yao ya ufadhili kwa IOC, kuhusu miradi wanayotaka kufanya.
Bach, amesema kutokana na hali ya mzozo huo kwa sasa, uchunguzi wa miradi hiyo na usambazaji wa fedha utaharakihwa.
Mwaka
uliopita, aliyekuwa rais wa IOC, Jack Rogge, alikamilisha ujumbe wake
wa kwanza kama mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
anayehusika na masuala ya vijana wakimbizi na michezo.
Maoni
Chapisha Maoni