MAN UTD TUMBO JOTO KWA MARTIAL
Anthony Martial ataweza akaigharimu klabu ya Manchester United £57.6m kama malipo hayatafanyika mapema.
Makamu
wa Rais wa Monaco Vadim
Vasilyev ameitahadharisha Manchester United kwamba huenda ikawa ni mara
tatu ya malipo ofa ya Anthony Martial ndani ya wiki, na akathibitisha
kuwa uhamisho wa mchezaji huyo unakaribia £58m.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 kwa sasa amefunga mabao 11 katika michezo 49 wakati akiwa na
Monaco, ameonekana kuwa mchezaji wa ghari mara baada ya kwenda Old Trafford akitokea Monaco katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili ambapo ilibainishwa kuwa gharama yake ni £36m.
Maoni
Chapisha Maoni