DAVID DEGEA TAYARI KURUDI KIKOSINI



David De Gea alianza katika mchezo wa Hispania dhidi ya Macedonia David de Gea amesema kuwa yeye anafurahia mpira wa miguu na yupo tayari kurudi katika kikosi cha Manchester United baada ya kuanzishwa kwa mara ya kwanza katika timu ya Taifa ya Hispania.

Goli kipa huyo ameachwa nje na kikosi cha kwanza cha United katika michezo yao minne ya kwanza ya ligi kuu Uingereza kutokana na tetesi zilizokuwa zikimhusisha kuhamia Real Madrid.

Hata hivyo baada ya uhamisho wake wa kwenda Hispania kwenda kombo hadi siku ya mwisho ya usajili, De Gea sasa mawazo yake ni kurudi katika kikosi cha kwanza ambapo namba yake imekuwa ikikaliwa na Sergio Romero ambaye hajafungwa mechi nne akicheza mechi sita katika mashindano yote.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii