MAN UTD MTIHANI KATIKA USAJILI
Rais wa kilabu ya Real Madrid
amesema Manchester United hawana uzoefu kuhusu kuhama kwa wachezaji na
ndiyo sababu uhamisho wa David De Gea ulitibuka.
Florentino Perez
aligusia pia kushindwa kwa United kusajili Fabio Coentrao kutoka Real na
Ander Herrera wa Athletic Bilbao siku
ya mwisho ya kuhama wachezaji
mwaka 2013.
Uhamisho wa De Gea ulitibuka kwa kuwa stakabadhi zake hazikuwasilishwa kwa wakati.
"Hawana uzoefu," Perez aliambia redio ya Uhispania ya Cadena SER.
"Jambo sawa lilitendeka kwa Coentrao na Herrera."
Real na United wamekuwa wakiwekeana lawama kwa kuchelewa kwa stakabadhi za kukamilisha uhamisho wa De Gea.
Kilabu
hiyo ya Uhispania inasema ilifanya kila ililoweza kumsajili mlinda
lango huyo wa miaka 24 kwa £29, lakini ikachelewa kwa dakika mbili.
United,
waliotaka kumsajili Keylor Navas kama sehemu ya mkataba huo, nao
walisema waliwasilisha stakabadhi zote dakika mbili kabla ya muda wa
mwisho kupita.
Perez alisema Red Devils walikubali tu kumuuza kipa
huyo saa 12 kabla ya soko la kuhama wachezaji kufungwa Uhispania, na
kisha wakachukua saa nane kurejesha stakabadhi.
Rais huyo wa Real pia alidai United walikuwa
wameonyesha ishara za kutaka kusajili mshambuliaji wa Wales Gareth Bale
pamoja na Wafaransa Karim Benzema na Raphael Varane kutoka kwao.
Makamu
mwenyekiti mtendaji wa United Ed Woodward alishindwa kuwasajili Herrera
na Coentrao majira ya joto ya 2013, wakati wake wa kwanza kuwa sokoni
baada ya kuchukua pahala pa David Gill.
Iliripotiwa kwamba
uhamisho wa Herrera ulivurugika baada ya matapeli, waliojidai
kuwakilisha United, kufika afisi za wasimamizi wa ligi ya Uhispania.
United waliambulia patupu kumchukua Coentrao baada yao kushindwa
kukamilisha uhamisho wake kwa wakati.
Kiungo wa kati huyo Herrera, 26, hatimaye alihamia kilabu hiyo ya Ligi ya Premia Juni 2014.
United wamesema watabadilisha sera yao ya uendeshaji shughuli sokoni na kuangazia zaidi wachezaji nyota siku za usoni.
Maoni
Chapisha Maoni