RAIS WA FIFA SEPP BLATTER ACHUNGUZWA
Rais wa shirikisho la soka duniani Fifa Sepp Blatter anachunguzwa na viongozi wa mashtaka nchini Uswizi.
Afisi ya mwanasheria mkuu wa serikali imesema Blatter anachunguzwa kwa “tuhuma za kuhusia katika usimamizi mbaya pamoja na – labda – tuhuma za kutumia vibaya pesa”.
Bw Blatter amehojiwa na pia afisi yake ikapekuliwa, Ofisi hiyo imesema.
Uchunguzi huo unahusu mkataba wa haki za utangazaji wa runinga ambao Blatter alitia saini pamoja na aliyekuwa mkuu wa soka wa eneo la Caribbea Jack Warner mwaka 2005.Bw Blatter pia anatuhumiwa kufanya “malipo yasiyo halali” mwaka 2011 kwa rais wa shirikisho la soka Ulaya Uefa Michel Platini, taarifa ya afisi hiyo imesema.
Mwezi Mei, maafisa saba wakuu wa Fifa walikamatwa Zurich kwa tuhuma za ufisadi kutoka kwa maafisa wa mashtaka nchini Marekani.
Blatter alishinda uchaguzi wa urais wa Fifa mara ya tano mfululizo Mei 29 lakini, baada ya tuhuma za ufisadi kukumba shirikisho hilo, alitangaza Juni 2 kwamba angejiuzulu.
Anatarajiwa kuondoka wadhifa wake wakati wa mkutano mkuu wa Fifa Februari 26.
Maoni
Chapisha Maoni