YANGA SC WAIENDEA BAGAMOYO COASTAL UNION, PATACHIMBIKA TAIFA JUMAPILI


MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga SC Jumatano wataingia kambini katika hoteli ya Kiromo, Bagamoyo mkoani Pwani kwa maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom mwishoni mwa wiki.Yanga SC wataanza na Coastal Union ya Tanga Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam- wakati mechi nyingine zote za ufunguzi zitachezwa Jumamosi. Katibu w Yanga SC, Dk Jonas Tiboroha amesema kwamba kwa siku mbili, leo na kesho timu itafanya mazoezi Dar es Salaam kabla ya kwenda Bagamoyo.
Yanga SC iliuanza vizuri msimu baada ya kutwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi wa penalti 8-7 dhidi ya Azam FC kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 
Tiboroha amesema kwamba baada ya wachezaji waliokuwa kwenye majukumu ya kimataifa kurejea wote, Jumatano timu itakwenda Bagamoyo. Na amesema wakiwa katika hoteli ya Kiromo, timu itakuwa inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani, nje kidogo ya Dar es Salaam. Yanga SC iliuanza vizuri msimu baada ya kutwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi wa penalti 8-7 dhidi ya Azam FC kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90- na sasa inaingia kwenye mbio za kutetea taji. Kabla ya Yanga SC na Coastal Jumapili, mechi za ufunguzi za Ligi Kuu Jumapili zitakuwa kati ya  Ndanda FC na Mgambo Shooting, African Sports na Simba SC, Majimaji FC na JKT Ruvu, Azam FC na Prisons, Stand United na Mtibwa Sugar, Toto Africans na Mwadui na Mbeya City na Kagera Sugar.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii