AZAM NA SIMBA KUPIGWA SHAMBA LA BIBI JUMAMOSI
MCHEZO
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kati ya Azam FC na Simba ya
Dar es Salaam, utafanyika Jumamosi Septemba 17, 2016 kama ilivyopangwa
awali.
Ila
mchezo huo utafanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam badala ya Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam kwa sababu za kuipa nafasi timu ya taifa ya
vijana ya mpira wa miguu ya Congo Brazzaville ambayo itakuwa nchini kwa
ajili ya mchezo wa ushindani dhidi ya wenyeji – Serengeti Boys ambayo ni
timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17.
Maoni
Chapisha Maoni