Karibu upate habari za michezo ya aina zote kwa haraka na uhakika. Utapata habari za soka, mpira wa kikapu, Tennis, mpira wa pete, masumbwi, mashindano ya magari, riadha na michezo mingine. Hapa utapata matokeo ya mechi mbalimbali, taarifa za wachezaji na timu zao.
MATOKEO EPL WEEKEND HII, LEICESTER HAISHIKIKI, MAN YAPIGWA 3
Pata kiungo
Facebook
X
Pinterest
Barua pepe
Programu Nyingine
Ligi kuu ya soka ya England imeendelea tena jumapili kwa michezo mitatu ,Sunderland wakicheza nyumbani dhidi ya vinara wa ligi Leicester city, waliambulia kipigo cha mabao 2-0, na kuwafanya leicester city kufikisha alama 72 katika Msimamo.Liverpool waliibamiza stoke city kwa kichapo cha mabao 4-1 yaliyofungwa na wachezaji Alberto Moreno, Daniel Sturridge na Divock Origi (mabao mawili) huku bao pekee la kufutia machozi la stoke city likifungwa na Bojan Krikic.
Mchezaji wa Liverpool Divock Origi akishangilia mara baada ya kuifungia timu yake goli la tatu dhidi ya Stoke City hapo jana
Na Mechi ya tatu ya mwisho kati ya Tottenham na Manchester united mchezo ulimalizika kwa United kuchabangwa mabao 3-0.
Dakika ya 70 mchezaji Dele Alli alianza kuiptia goli bao la kwanza Tottenham .
Erik Lamela wa Tottenham Hotspur akishangilia mara baada ya kuifungia timu yake goli la tatu
Tottenham iliandika bao la pili kupitia kwa Toby Alder-weireld, huku bao la tatu likipachikwa na Erick Lamela dakika ya 76.
Ikiwa leo ni Septemba 21, 2016 magazeti ya leo yamekuja na habari kadha wa kadha ikiwemo ile ya Ajali mbaya, mwamuzi kiboko apewa Yanga vs Simba na kwenye burudani Alikiba Helikopta Diamond
Chelsea imefanikiwa kumsajili Michy Batshuayi Michy Batshuayi amefanikiwa kujiunga na Chelsea baada ya kukamilika kwa vipimo vya afya huko Bordeaux, chanzo cha Sky kimeripoti
Julai 13 2016 naanza kwa kukusogezea post ya stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye, Udaku , Michezo na siasa ili ujue kinachoendelea mtu wangu.. usiache kukaa karibu yangu kwenye facebook, twitter na instagram @ cauntermgaya ili niwe nakutumia kila kinachonifikia
Maoni
Chapisha Maoni