MADEAMA WATUA DAR KUVAANA NA YANGA
Wapinzani wa klabu
ya Young Africans, katika michuano ya kuwania Kombe la Shirikisho
Barani Afrika, Medeama kutoka Ghana, wametua Dar es Salaam tayari kwa
mechi baina ya timu hizo Jumamosi.
Wachezaji hao waliwasili Dar Alhamisi na wakafanya mazoezi katika uwanja wa Karume.
Yanga itaikaribisha Medeama kwa mchezo wa tatu kuwania taji hilo hatua ya makundi katika uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Mchezao huo utaanza saa 10.00 jioni
Michezo
miwili ya awali ya Yanga katika michuano hiyo ilikuwa ni dhidi ya Mo
Bejaia ya Algeria ambako ilipoteza kwa bao 1-0 kabla ya kupoteza tena
dhidi ya TP Mazembe, mechi iliyopigwa jijini Dar es Salaam.
Mchezo
wa Jumamosi utachezeshwa na waamuzi kutoka Misri ambao ni Ibrahim Nour
El Din atakayekuwa mwamuzi wa kati; akisaidiwa na Ayman Degaish na Samir
Gamal Saad wakati mwamuzi wa akiba akiwa ni Mohamed Maarouf Eid
Mansour, kwa mujibu wa Shirikisho la Kandanda la Tanzania (TFF).
Maoni
Chapisha Maoni