WENGER APEWA MKATABA WA MIAKA 2 ARSENAL
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger
amekubali kuchukua mkataba wa miaka miwili katika klabu hiyo, hatua
itakayoendeleza muda ambao amekaa katika klabu hiyo
.
Mfaransa huyo amekuwa meneja wa Arsenal kwa miaka 21 sasa.
Wenger
na mmiliki wa klabu hiyo Stan Kroenke walikutana Jumatatu kuamua hatima
ya meneja huyo, na kisha uamuzi wao ukawasilishwa kwa mkutano wa bodi
Jumanne.
Arsenal wanapanga kutangaza rasmi uamuzi huo Jumatano.
Gunners
walimaliza Ligi ya Premia wakwia nafasi ya tano, mara yao ya kwanza
kumaliza chini ya nafasi ya nne tangu Wenger alipojiunga nao mwaka 1996.
Walimaliza
alama 18 nyuma ya mabingwa Chelsea, lakini walifanikiwa kuwachapa Blues
katika fainali ya Kombe la FA uwanjani Wembley Jumamosi.
Mkataba wa Wenger ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu
Wenger aliongoza Gunners kushinda mataji matatu ya Ligi ya
Premia na pia vikombe vinne vya FA misimu yake tisa ya kwanza kwenye
usukani.
Mwaka 2003-04, aliibuka meneja wa kwanza tangu 1888-89 kuongoza timu iliyomaliza ligi kuu bila kushindwa.
Lakini
baada ya kushinda Kombe la FA mwaka 2005, walisubiri kwa miaka mingine
tisa - sawa na siku 3,283, kabla ya kushinda kikombe kingine.
Walilaza Hull City fainali ya Kombe la FA mwaka 2014 na kisha wakashinda kikombe hicho tena mwaka uliofuata.
Baadhi
ya mashabiki wa Arsenal wamekuwa wakimtaka Mfaransa huyo mwenye umri wa
miaka 67 ajiuzulu, hasa baada ya matokeo mabaya msimu huu. Shutuma
zaidi zilitolewa waliposhindwa kwa jumla ya mabao 10-2 na Bayern Munich
katika hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwezi Machi.
Walimaliza msimu wakiwa wameshinda mechi tano
mfululizo, lakini matokeo hayo hayakutosha kuwawezesha kuwapita
Liverpool waliomaliza nafasi ya nne na kujaza nafasi ya mwisho ya
kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Jumamosi, Wenger aliambia BBC
kwamba shutuma na uokosoaji aliokumbana nao msimu huu ni wa
"kufedhehesha" na kwamba hatawahi kuusahau kamwe maishani
Maoni
Chapisha Maoni