TIGER WOODS ASHUTUMIWA KWA ULEVI
Siku moja baada ya mchezaji nyota wa
gofu Tiger Woods kukausha kuwa hakuwa amelewa wakati polisi
walipomkamata siku ya jumatatu, taarifa za polisi zinasema kuwa mchezaji
huyo alikutwa amelala ama (amezima) wakati injini ya gari ikiwa
inafanya kazi
.

Kwa
mujibu wa taarifa hizo, Woods mchezaji wa zamani namba moja kwa ubora
duniani, alikutwa katika usukano wa gari yake aina ya Mercedes na
aliamshwa kwa dakika kadhaa na afisa wa polisi aliyemuona.
Alikamatwa
kwa kosa la kuendesha chombo cha moto akiwa amelala lakini alikanusha
hilo na kusema kuwa ni matokeo ya dawa kali anazozitumia baada ya
kufanyiwa upasuaji wa mgongo.
Maoni
Chapisha Maoni