HAMOU AFUNGIWA KUCHEZA FRENCH OPEN KWA KUMBUSU MWANDISHI WA HABARI

Mchezaji wa Tenisi Maxime Hamou amefungiwa kushiriki michuano ya French Open mjini Paris, baada ya kujaribu kumbusu mwandishi wa habari mara kadhaa wakati wa mahojiano
.
Hamou katikati akiwa ameinama kumbusu Maly Thomas
Mfaransa huyo mwenye miaka 21 alijaribu kumbusu Maly Thomas huku akiwa amemshika mabega yake na shingo licha ya mwanadada huyo kukataa mara kwa mara.
Alikuwa akihojiwa siku ya jumatatu baada ya kupoteza mchezo wake katika mzunguko wa kwanza.
Katika taarifa yake, chama cha Tenisi nchini Ufaransa kimesema kitendo hicho ni cha kukemewa kwa nguvu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii