CHELSEA YATWAA UBINGWA WA HISTORIA ENGLAND

 expanded thumbnail
Mabingwa wa Premier League Chelsea wameinyuka Sunderland 5-1 siku ya jana Jumapili wakati nahodha John Terry akiwaaga tayari kuondoka Stamford Bridge
.
Mkongwe huyo wa The Blues, ambaye ameitumikia Chelsea kwa miaka 22 ataondoka majira haya ya joto, jumapili alicheza dk 26 baada ya kuanzishwa na baadae kupumzishwa kwa namna ya aina yake ya kupongezwa na wachezaji wenzake na kila aliyehudhuria mechi hiyo.
 
Willian alisawazisha dk (8) akifuta goli la mapema lililofungwa na Javier Manquillo kunako dk 3, baadae magoli manne yakifungwa na Eden Hazard dk(61), Pedro dk(77) na magoli mawili ya Michy Batshuayi aliyetokea benchi(90, 90+2) na kuifanya kuandika rekodi ya kushinda mechi 30 za Premier League msimu huu.
Ushindi wa jana ulikuwa muhimu kwao kwani ndio siku waliyokabidhiwa kombe la ligi na wanasubili fainali ya FA Cup dhidi ya Arsenal Jumapili.

Diego Costa reacts during the match
Diego Costa

Chelsea imekuwa ni timu pekee kwa kumaliza ligi kwa kushinda michezo 30 kati ya 38 ya ndani ya msimu, hivyo wamevunja rekodi ya wao wenyewe ya misimu ya 2004/05 na 2005/06

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii