ARSENAL WASHINDWA KUFUZU UEFA
Arsenal imeshindwa kufuzu kwa kombe la klabu bingwa barani ulaya,
Champions League kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20 licha ya
ushindi wake dhidi ya Everton wa mabao 3-1 katika siku ya mwisho ya
mechi za Primia League.
Arsenal ilianza mechi vizuri ikiwa pointi
moja nyuma ya Liverpool na walikuwa katika nafasi bora kuchukua nafasi
yao wakati waliongoza mnamo dakika ya nane.
Lakini ukakamavu wa Liverpool uliiwezesha kusalia katika timu nne za kwanza baada ya kuwatandika Middlebrogh mabao 3-0.
Manchester City ilishika nafasi ya tatu baada ya kuinyuka Watfoird mabao 5-0.
Maoni
Chapisha Maoni