MATOKEO UEFA: LEICESTER, MADRID ZA SHINDA

Usiku wa kuamkia leo ulikuwa ni usiku wa UEFA Champions League ambapo timu mbali mbali kutoka katika makundi ya E, F, G na H walijitupa uwanjani kupepetana ili kila mmoja kuhakikisha anaibuka na alama tatu muhimu ikiwa ni michezo ya kukamilisha mzunguko wa kwanza
. Michezo hiyo ambayo yote ilichezwa majira ya saa 3:45 za usiku tulishuhudia Real Madrid wakiibuka na ushindi mnono wa mabao 5-1 dhidi ya Legia Warszawa Fc kwenye dimba la Bernabeu. Nao Leicester City wameendelea kufanya vizuri kwenye michuano hizo kwa kuweka rekodi ya kuwa timu pekee ambayo haijapoteza hata alama moja wakiwa na alama 9 katika michezo mitatu mara baada ya jana kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya FC Copenhagen, goli pekee lililofungwa na Mahrez mnamo dk 40
ya mchezo.
MATOKEO MENGINE
Group E
Bayern Leverkusen 0-0 Tottenham Hotspurs
CSK moscow 1-1 Monaco
Group F
Real Madrid 5-1 Legia Warszawa
Sporting CP 1-2 borussia Dortmund
Group G
Club Brugge 1-2 FC Porto
Leicester City 1-0 FC Copenhagen
Group H
Dinamo Zagreb 0-1 Sevilla
Lyon 0-1 Juventus


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii