ANDER HERRERA 'MAN OF THE MATCH' LIVER VS MAN UTD

Image result for ANDER HERRERA
Mchezo wa kusisimua wa ligi kuu ya soka England umemalizika kwa suluhu ya bila kufungana.
Katika mchezo huo kipindi cha kwanza timu zote zilishambuliana kwa zamu huku kipindi cha pili Liverpool ikishambulia zaidi lango la United
.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa hakukasirika lakini pia hakufurahishwa na kiwango cha uchezaji wa timu yake.
Klopp pia ameisifu safu ya ulinzi ya Man U na kusema ilikuwa vigumu kushinda kutokana na ulinzi ulivyokuwa imara.
Kwa upande wake meneja wa Man U Jose Mourinho amesema licha ya kutopata matokeo aliyoyataka lakini ameridhishwa na matokeo hayo.
Amesema si matokeo mabaya kwani waliweza kumzuia hasimu wao wa jadi kuondoka na alama tatu nyumbani kwake.Image result for LIVERPOOL VS MAN UTD

Katika mchezo huo Ander Herrera aliibuka kuwa mchezaji bora huku akiwa mchezaji aliyegusa mpira mara nyingi kuliko mchezaji yoyote , aligusa mpira mara tisini
Image result for ANDER HERRERA
Ander Herrera mchezaji bora wa mechi ya jana kati ya Liverpool na Man Utd akitoa pasi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii