MWANASOKA WA SIERRA LEONE,'BAH' AFARIKI DUNIA
Aliyekuwa mwanasoka
wa kimataifa, raia wa Sierra Leone, Mamadu Alphajor Bah amefariki
dunia katika ajali mbaya ya barabarani iliyofanyika karibu na mji mkuu
wa nchi hiyo Freetown
.
Gari la mchezaji huyo wa kiungo kati aliye na umwi wa miaka 39 liligongana na lori uso kwa uso wakati wa ajali hiyo.
Alikimbizwa
hospitalini Goderich, lakini akafariki punde kutokana na kupoteza damu
nyingi. Polisi wangali wanachunguza ajali hiyo.
Bah aliwahi kuichezea nchi yake Sierra Leone mara 25 katika mechi za kimataifa.
Mchezaji
mashuhuri Mohamed Kallon, aliyekuwa nahodha wa timu hiyo wakati Bah
alipokuwa angali anacheza, amelitaja tukio hilo kama pigo kuu.
"
Bado nimeshikwa na mshtuko, na nina huzuni sana kumpoteza kaka na
rafiki yangu Mamadu Alphajor Bah," Kallon ameiambia BBC. "Alikuwa
mchezaji mwenye kipaji kizuri, mtu anaejituma, mcheshi , unaefurahiwa
kuwa nae katika timu moja .
Mchezaji mwenzake mwengine Ibrahim
Kargbo,nae amesema : 'Ni kama ndoto mbaya , kweli nimeshtuka, ni kaka
ambae daima atakuwa nasi kwenye fikira zetu, Mungu amweke mahala pema
peponi ''.
Bah alisifika sana kama mmojawapo wa wachezaji bora wa timu ya taifa la Sierra Leone hasa katika miaka ya 2000 hadi 2008.
Katika
ngazi ya klabu , aliichezea timu ya ubelgiji ya KSC Lokoren hapo
1994-96 kabla ya kuelekea Korea kusini kuichezea Chunnam Dragons hapo
1997.
Miaka miwili baadae alielekea UChina na kuwa raia wa kwanza
wa Sierra Leone kucheza katika ligi kuu itwayo Chinese Super league,
akiwa katika klabu ya Xiamen Lanshi mwaka wa 1999-2003 kisha akahamia
klabu ya Zhejiang Lucheng hapo 2004.
Maoni
Chapisha Maoni