MATOKEO UEFA

 Alexis Sanchez celebrates after scoring for Arsenal against PSG
Usiku wa jana ulikuwa wa aina yake kwani mafahali walikuwa wakipambana katika viwanja mbalimbali lakini kwa upande wa mtanange wa PSG vs Arsenal palikuwa hapatoshi kwani Alexis Sanchez aliwasaidia Arsenal kuondoka
na alama moja mechi yao ya kwanza msimu huu Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Paris St-Germain.
Edinson Cavani aliwaweka PSG mbele baada ya sekunde 42 pekee na alikuwa na nafasi ya kufunga mabao matatu kufikia muda wa mapumziko.
Alikosa bao wazi baada ya kumchenga David Ospina lakini akatuma kombora lake nje na baadaye kidogo akashindwa kufunga bao rahisi.
Sanchez alifunga bao kwa kutumia vyema mpira uliodunda baada ya Arsenal kupata kombora la kwanza kabisa la kulenga goli.

Alex Iwobi alikuwa na fursa ya kufungia Arsenal bao la ushindi dakika za mwisho lakini akashindwa.
Nyota wa Arsenal Olivier Giroud na Marco Verratti wa PSG walioneshwa kadi nyekundu.
Goli la PSG lilifungwa na Edson Cavan katika dakika ya kwanza ya mchezo
 David Ospina made some vital saves for Arsenal
Katika mechi nyingine Celtic walipokea kichapo kibaya zaidi katika mashindano ya Ulaya Jumanne usiku baada ya kuchapwa mabao 7-0 na Barcelona uwanjani Camp Nou.
 Lionel Messi celebrates scoring the first of his three goals as Barcelona thrashed Celtic at the Nou Camp
Mshambuliaji Lionel Messi, raia wa Argentina, alifunga 'hat-trick' yake ya sita katika mechi hiyo ya kundi C.
Nahodha wa Celtic Scott Brown akiwashukuru mashabiki baada ya mechi dhidi ya Rangers

MATOKEO YA MECHI ZA JANA
  •   Barcelona 7 - 0 Celtic 
  •   Bay Munich 5 - 0 Rostov 
  •   PSG 1 - 1 Arsenal 
  • Benfica 1 -1 Besiktas 
  • Dynamo Kiev 1- 2 Napoli
  • Bay Munich 5- 0 Rostov 
  • PSV 0- 1 A Madrid 
  • Basel 1 - 1 Ludogorets 

Mechi za leo Septemba 14, 2016

  •   Club Brugge 19:45 Leicester
  •   Man City 19:45 M'gladbach
  •   R Madrid 19:45 Sporting
  •   Tottenham 19:45 Monaco
  •  

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii