MATOKEO EPL: MAN CITY, ARSENAL, LEICESTER ZASHINDA


Manchester City roared past Bournemouth

 Manchester City ikiwa nyumbani katika uwanja wa Etihad ilifanikiwa kuibamiza Bournemouth jumla ya mabao 4-0 na hivyo kudhihirisha kwamba ipo vizuri kwa asilimia 100 katika mechi za mwanzo wa msimu
huu.
Katika pambano lingine Alexis Sanchez alizama wavuni mara mbili na kukosa penalti moja wakati Arsenal ikiigaragaza Hull City bao 4-1, Hull alikuwa nyumbani.
Everton 3-1 Middlesbrough
Nao Everton wameendelea kuonesha ubaora wao wa kutopoteza mechi wakiwa chini ya Ronald Koeman katika mechi tano za mwanzo mara baada ya hapo jana kutoka nyuma na kuilaza Middlesbrough 3-1 kwenye uwanja wa Goodison Park.
Leicester 3-0 Burnley
Katika mtanange wa Leicester vs Burnley, Islam Slimani umeonesha ubora wake ikiwa ni mechi yake ya kwanza EPL baada ya kutupia mabao mawili wakati Leicester ikiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Burnley.

West Brom wlionesha uwezo wa hali ya juu katika mechi yao ya jana jumamosi walipo ilaza West Ham 4-2 kwenye uwanja wa Hawthorns.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii