LIVERPOOL YAISULUBISHA CHELSEA, YAIPIGA KWAO

Jordan Henderson alifunga goli la msimu usiku wa leo wakati Liverpool ikiicharaza Chelsea 2-1 katika dimba la Stamford Bridge.
Kikosi cha Jurgen Klopp kilionekana kuwa na nguvu zaidi kipindi cha kwanza ambapo nguvu hiyo iliwasaidia kuwapiga wapinzani wao goli mbili, magoli yalifungwa na Dejan Lovren na Henderson.
Chelsea, baada ya kurudi kutoka mapumziko walijitahidi kubadili mchezo na kufanya Diego
Costa kupata goli lake la tano katika msimu huu mnamo dakika ya 29
![]() |
Diego Costa akiifungia Chelsea |
huku
Liverpool wakipoteana hali iliyowafanya warudi nyuma kulinda.
Maoni
Chapisha Maoni