DAVID LUIZ KUCHEZA MECHI DHIDI YA LIVERPOOL
Kocha wa Chelsea Antonio Conte, amethibitisha kuwa David Luiz atarudi uwanjani akiwa na kikosi cha Chelsea kwa mara ya pili katika mechi dhidi ya Liverpool usiku wa kesho
Ijumaa.John Terry aliondoka uwanjani Liberty Stadium akiwa anachechemea siku ya Jumapili. |
Luiz atachukua nafasi ya John Terry kwenye kikosi cha The Blues, hii ni baada ya Terry kuumia enka ya mguu wakati wakidroo 2-2 na Swansea siku ya Jumapili na atakuwa nje kwa siku 10.
Nyota huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 29 aliondoka Stamford Bridge miaka miwili iliyopita na kuelekea Ufaransa kwa dau la Uero 50 millioni ambayo ilibaki kuwa ni rekodi kubwa kuwahi kutokea kwa mauzo ya beki.
Kwa miaka mitatu aliyokaa klabuni hapo iliyoko magharibi mwa London, Luiz amecheza mechi 143 na kufunga magoli 12 katika michuano yote.
Conte amesema: "Unaposajili mchezaji mpya unatakiwa kumuacha ili aweze kuendana na mfumo unaotaka na pia kuelewana na wachezaji wenzake".
Chelsea vs Liverpool
Septemba 16, 2016, 2:30 usiku
Live kwenye
Maoni
Chapisha Maoni