DANGOTE KUINUNUA ARSENAL
Aliko Dangote, mtu
tajiri zaidi barani Afrika,ana mpango wa kuinunua klabu ya Arsenal
kutoka nchini Uingereza katika kipindi cha miaka minne.Dangote
ambaye ni raia wa Nigeria ana thamani ya dola bilioni 10.9,
kulingana na
orodha ya watu tajiri duniani iliotolewa na runinga ya Bloomberg mjini
New York siku ya Jumatano, alitangaza nia yake ya kukinunua klabu hicho
mwaka uliopita.
Alisema kuwa anasubiri biashara zake kuimarika
pamoja na uwekezaji wake wa ujenzi wa bomba la gesi na kiwanda cha
kusafisha mafuta kabla ya kukinunua klabu hicho.
Arsenal |
''Hakuna tatizo
kwamba atakinunua klabu hicho'' na si tatizo la fedha ,alisema Dangote
katika mahojiano na runinga ya
''Pengine miaka mitatau au mine.Swala ni kwamba
tunachangamoto nyingi.Ninahitajika kukabiliana nazo mwanzo baadaye
nitaangazia swala la ununuzi huo''.
Dangote ambaye ni shabiki
mkubwa wa Arsenal amepoteza kiasia cha dola bilioni 4.4 mwaka huu
kutokana na kushuka kwa thamani ya sarufi ya Nigeria.
Utajiri wake mwingi upo katika kiwanda cha simiti cha mjini Lagos.
Iwapo atainunua timu hiyo basi atakuwa mtu wa kwanza kutoka barani Afrika kumiliki timu iliopo katika ligi kuu ya Uingereza.
Maoni
Chapisha Maoni