WILLIAN ASAINI MIAKA MINNE CHELSEA
Willian aendelea kutumikia maisha yake ya soka Chelsea
Mshambuliaji wa Chelsea Willian amesaini mkataba wa miaka minne ili kuendelea kubakia Stamford Bridge.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 alichaguliwa kuwa mchezaji bora ndani ya chelsea katika msimu wa 2015/16 na mashabiki pamoja na wachezaji wenzake na hivyo sasa atakaa pale mpaka 2020.
Willian amefunga mabao 19 katika mechi 140 arobaini alizoichezea Chelsea tangu afike Stamford Bridge akitokea Urusi katika klabu ya Anzhi Makhachkala kwa dau la £32m mwaka 2013.
Maoni
Chapisha Maoni