URENO MABINGWA EURO 2016 WAICHAPA UFARANSA 1-0 (PICHA)

Cristiano Ronaldo was taken off injured but Portugal still lifted the trophy
Licha ya Cristiano Ronaldo kutolewa nje kwa baada ya kuumia lakini Ureno wamechukua kombe.
Ureno wametwaa ndoo ya Euro 2016 baada ya mchezaji wa akiba Eder kuingia na kuwapatia goli katoka dakika za nyongeza na hivyo kufanya matokeo kuwa 1-0 dhidi ya wenyeji Ufaransa
katika mtanange uliopigwa mjini Paris, licha ya nahodha wao Cristiano Ronaldo kutolewa nje baada ya kuumia katika kipindi cha kwanza.
Ronaldo attempted to continue, but eventually came off in tears
Mshambuliaji wa zamani wa Swansea Eder, ambaye aliingia kwa kuchelewa katika kipindi cha pili mara baada ya kutolewa kwa Renato Sanches, alipiga shuti dogo ambalo lilikuwa likilenga posti ya chini huku akimuacha golikipa Hugo Lloris akigaragara na asiambulie kitu.
Eder of Portugal celebrates scoring the winning goal in Paris
Ureno hii ni mara yao ya kwanza kuchukua kombe kubwa kama hili.
Nahodha wa Ureno Ronaldo alionekana kutokwa na machozi mara baada ya kuumia goti mnamo dk 25 kipindi cha kwanza hali iliyowatia hofu mashabiki wa Ureno lakini mpira unadunda.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii