UFARANSA YAISAMBARATISHA ICELAND
Ufaransa imefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali baada ya kuipa kichapo cha bao 5-2 timu ya Iceland hapo jana usiku.
Iceland wameondoka
katika Euro lakini kwa hakika watabaki katika vinywa vya wapenzi wa
Soka. Nahodha wao Aron Gunnarsson amesema kwa hakika huu ni mwanzo wao
wa kuanza kukwea jukwaa la kimataifa.
Pogba akiifungia Ufaransa bao la pili |
Anasema kile walichokipata jana katika Stade de France kimewasikitisha lakini wanajivunia ushiriki wao kwani umewajenga sana.
Payet akiifungia timu yake ya taifa bao la tatu |
Sasa
wanajipanga katika kuwania kufuzu kushiriki kwa mara ya kwanza katika
kombe la Dunia litakalofanyika Urusi mwaka 2018 wakiwa kwenye kundi
ambalo lina Croatia, Ukraine, Finland, Uturuki na Kosovo.
Giroud akishangilia goli lake la pili |
Inakadiriwa asilimia 10 ya Raia wote wa nchi walikuwa wamesafiri kuja kuishabikia timu yao.
Michuano
hii pia imetumika kuwatangaza wachezaji na sasa tutaanza kukona
wakienda huku na kule, kwa mfano mshambuliaji Hal Robson Kanu wa Wales
ambaye ameachwa huru na Reading mwishoni mwa msimu wa 2015-16 hivi sasa
ameanza kutakiwa huku na kule na hasa baada ya bao lake lile alilogeuka
katika kumi na nane akawabamiza ubelgiji na kuipeleka Wales nusu
fainali.
Maoni
Chapisha Maoni