TOTTENHAM YAMSAJILI VINCENT JANSSEN

 

Tottenham imemsajili Vincent Janssen katika dili la miaka minne

Tottenham imekamilisha usajili wa Vincent Janssen kutoka AZ Alkmaar katika mkataba wa miaka minne.

 
Mdachi huyo mwenye umri wa miaka 22 amekamilisha vipimo vya afya jumatatu na sasa imethibitishwa rasmi kuwa atasaidiana na Harry Kane pale Spurs katika nafasi ya ushambuliaji msimu ujao, ada yake ni £18.6m. 
Janssen alitwaa tuzo ya mfungaji bora akiwa na mabao 27 msimu uliopita na hivi sasa ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Uholanzi ambayo inatarajia kupambana na  England pale Wembley, mwezi March.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii