TANZANIA NA KENYA ZAPANDA VIWANGO FIFA
Kenya imepanda
hatua 43 katika orodha ya hivi punde zaidi ya shirikisho la soka duniani
FIFA na kuorodheshwa katika nafasi ya 86 duniani
.
Hii ni kwa
mujibu wa orodha ya FIFA inayoonesha kuwa Algeria imesalia kidedea
barani Afrika japo inaorodheshwa katika nafasi ya 32 duniani.
Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ndiyo inayoongoza katika kanda ya afrika mashariki na kati.
DR Congo imeorodheshwa katika nafasi ya 59 duniani na 9 barani Afrika.
Uganda
Cranes inaorodheshwa katika nafasi ya 15 barani Afrika na nafasi ya 69
duniani nafasi mbili mbele ya vigogo ya soka barani humu Nigeria.
Kenya ambayo ndilo taifa lililoimarika zaidi inaorodheshwa katika nafasi ya 86.
Harambee
stars ya Kenya iliyojifurukuta na kuilaza Congo Brazzaville iliimarika
hatua 43 na kuingia chini ya mataifa bora 100 kwa mara ya kwanza katika
kipindi cha miezi sita.
Aidha hii ndiyo nafasi ya juu zaidi kwa Kenya tangu mwaka wa 2008.
Amavubi Stars ya Rwanda imeshuka hatua 8 na kuorodheshwa katika nafasi 111 duniani.
Licha ya kupanda hatua 13, Taifa Stars ya Tanzania inaorodheshwa katika nafasi ya 123
Inafatwa kwa karibu na Burundi ambayo vilevile imepanda hatua 7 na kutimia nafasi ya 125.
Ethiopia ni ya 132,
Sudan 142
Sudan Kusini 153
Mataifa
ya mwisho kabisa katika orodha hiyo ya FIFA ni mataifa ya kanda ya
Afrika Mashariki yaani Djibouti, Eritrea na Somalia ambazo zote
zinaorodheshwa katika nafasi ya 205.
Argentina ingali inaongoza duniani ikifwatwa na Ubeljiji.
Orodha ya mataifa kumi bora barani Afrika
Algeria (32)
Ivory Coast (35)
Ghana (36)
Senegal (41)
Misri (43)
Tunisia (45)
Cameroon (53)
Morocco (54)
DR Congo(59)
Mali (61)
Orodha ya mataifa kumi bora duniani
1 Argentina
2 Ubeljiji
3 Colombia
4 Ujerumani
5 Chile
6 Ureno
7 Ufaransa
8 Spain
9 Brazil
10 Italia
Maoni
Chapisha Maoni