SHEVCHENKO ATEULIWA MENEJA UKRAINE

Ukraine imemteua mshambuliaji wa zamani wa AC Milan na Chelsea Andriy Shevchenko kuwa meneja mpya wa timu ya taifa.
Shevchenko, 39, aliyechezea timu ya taifa mara 111, atajaza nafasi ya Mykhaylo Fomenko, aliyeondoka baada ya taifa hilo kuondolewa michuano ya Euro 2016 katika hatua ya makundi.

Shevchenko alikuwa msaidizi wa Fomenko Ukraine waliposhindwa mechi zao zote dhidi ya Ujerumani, Ireland Kaskazini na Poland.
Mchezaji huyo wa zamani wa Dynamo Kyiv, aliyestaafu mwaka 2012, hajawahi kuhudumu kama meneja awali.
Shevchenko
Shevchenko (kushoto) alipokuwa anachezea Chelsea
Ukraine's record scorer with 48 goals, Shevchenko ndiye anayeshikilia rekodi ya ufungaji mabao timu ya taifa ya Ukraine na alikuwa nahodha walipofuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2006.
Ametia saini mkataba wa miaka miwili.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii