URENO YATINGA NUSU FAINALI EURO

Ureno imetinga
hatua ya nusu fainali katika michuano ya Euro inayoendelea nchini
Ufaransa na kuwa nchi ya kwanza kufuzu katika hatua hiyo baada ya
kuwafunga Poland kwa mikwaju ya penalti 5-3.
Dakika 120 zilishuhudia mchezo huo ukiisha kwa suluhu ya goli 1-1.


Ricardo Quaresma alikuwa shujaa kwa timu yake baada ya
kupiga penalti ya mwisho iliyoivusha katika hatua nyingine huku kiungo
wa Jakub Blaszczykowski akikosa mkwaju wa penalti kwa upande wa Poland.
Ureno itakutana katika hatua ya nusu fainali na mshindi wa mchezo kati ya Wales na Ubelgiji.
Maoni
Chapisha Maoni