MANE KUJIUNGA NA LIVERPOOL RASMI

Sadio Mane is having a medical at Liverpool


Sadio Mane anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya kwaajili ya kujiunga na klabu ya vijogoo wa Anfield Liverpool,  ambapo gharama yake inasadikaka kuwa itakuwa kati ya £34m - hadi £36m akitokea Southampton.
 Dili hilo la kumsainisha Mane linaweza kukamilika katikati mwa wiki hili, na hivyo kumfanya kuwa ni mchezaji wa tano kujiunga na Liverpool akitokea Southampton ndani ya misimu mitatu.
Wengine ni Dejan Lovren, Adam Lallana na Nathaniel Clyne ambao bado wapo Anfield, huku Rickie Lambert akiwa tayari ameshatimkia West Brom baada ya msimu mmoja tu.

Mane has scored 21 goals in 67 Premier League games for Southampton
Nyota huyo wa timu ya taifa ya Senegal katika ligi kuu Uingereza amefunga jumla ya mabao 21 katika mechi 67 mara baada ya kujiunga na watakatifu hao akitokea Red Bull Salzburg miaka miwili iliyopita.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii