MATOKEO LALIGA; MADRID APIGA 4, BARCA ACHEZEA KICHAPO

Ligi kuu Hispania ali maarufu kama LALIGA imeendelea mwishoni mwa wiki hii ambapo timu takribani timu 8 zilijitupa ndani ya viwanja 4 kila mmoja akisaka alama 3 muhimu kwani mara baada ya mechi za lero kila timu itakuwa imebakiza michezo sita pekee.
 
Real Madrid katika mtanange wao wa mapema wakiwa nyumbani wamefanikiwa kuigaragaza Eibar kwa kalamu ya magoli 4-0, mabao ya Madrid yametiwa kimyani na James Rodriguez (5), Lucas Vazquez (18), Cristiano Ronaldo (19),Jesse Rodriguez (39).
Jesse akishangilia goli lake lililokamilisha karamu ya mabao 4-0 dhidi ya Eibar
 Wakati mjini Madrid wakisherekea ushindi hali imekuwa mbaya kwa wapinzani wao ambao wanaongoza ligi Barcelona ambapo wakiwa ugenini mbele ya Real Sociedad wameambulia kipigo cha goli 1-0, goli lililotupiwa kambani na kijana mdogo kabisa Mikel Oyarzabal 
Mikel Oyarzabal akishangilia goli
 
Matokeo hayo yanaifanya Real kuwa nyuma ya vinara wa La Liga Barcelona kwa alama nne tu!.
Lionel Messi akiwa amechukia mara baada ya timu yake kupokea kipigo

Barcelona haijashinda katika mipambano yake yote sita ambayo imechezwa katika uwanja wa Anoeta Stadium, kwani wamepoteza mara tano na ushindi wa mwisho ulikuwa kipindi cha kocha Frank Rijkaard mwaka 2007.
 
MATOKEO
 
FT Real Madrid 4 - 0 Eibar

FT Espanyol 1 - 3 Atletico Madrid

FT Real Sociedad 1 - 0 Barcelona

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii