MATOKEO EPL , ARSENAL YASIMAMISHWA!

 
Weekend hii ligi kuu ya England imeendelea kwa nyasi kupata shida katika viwanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile mechi ya mapema ya West Ham dhidi ya Arsenal iliyopigwa majira ya saa 8:45 mchana na mechi ya usiku majira ya saa 1:30 Man City dhidi ya
Westbromwich Albion

Katika mtanange ulioisha kwa timu kufungana mabao 3-3 wa West Ham walio wakaribisha Arsenal Andy Caroll ameibuka gumzo mara baada ya kutupia hatrick ndani ya dk 10 pekee
 
 Andy Caroll akipachika goli la pili kwa tikitaka safi mbele ya mabeki wa Arsenal

Andy Caroll alifunga mabao matatu na kuiwezesha West Ham kuizuia Arsenal na hivyobasi kuvunja matumaini ya timu hiyo kushinda taji la ligi ya Uingereza.

Arsenal sasa iko pointi 10 nyuma ya Leicester ikiwa imesalia mechi sita.

Mesut Ozil na Alexis Sanchez waliiweka Arsenal kifua mbele kufuatia pasi nzuri za Iwobi ,lakini Caroll alifunga mabao mawili ya ghafla ndani ya sekunde 160 ili kusawazisha.

Kichwa kizuri katika kipindi cha pili kilimpatia Andy Caroll bao lake la tatu ,kabla ya beki wa Arsenal Laurent Koscielny kusawazisha.

Hatahivyo West Ham iliongeza rekodi yake ya kutofungwa katika ligi ya Uingereza na kufikia mechi 14 wakiwa nyumbani ,lakini kikosi hicho cha kocha Slaven Bilic kinasalia nafasi ya sita katika jedwali la ligi ya Uingereza.

MATOKEO YA MECHI NYINGINE
 
FT Aston Villa 1 - 2 AFC Bournemouth

FT Crystal Palace 1 - 0 Norwich City

FT Southampton 3 - 1 Newcastle United

FT Swansea City 1 - 0 Chelsea

FT Watford 1 - 1 Everton

FT Manchester City 2 - 1 West Bromwich Albion 

MECHI ZA KESHO
15:30
Sunderland
VS
Leicester City

18:00
Liverpool
VS
Stoke City
18:00
Tottenham Hotspur
VS
Manchester United

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii