IBRAHIMOVIC KUJIUNGA NA MAN UTD



  Zlatan Ibrahimovic ameonesha nia ya kutaka kujiunga na kikosi cha Manchester United katika majira ya joto lakini kama kocha wa klabu hiyo Louis van Gaal ataondoka.

Ibrahimovic atamaliza mkataba wake na klabu ya Paris St Germain(PSG) mwishoni mwa msimu huu na hivyo ananafasi ya kuchagua kujiunga na klabu yeyote ya Ulaya au kwenda ligi ya China.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari mwezi March alieleza kuwa anavutiwa na kucheza ligi ya Uingereza na kwa kifupi alikuwa anamaanisha kuchezea Man United kama Mreno Mourinho atapewa timu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii