ESPERANCE YAKIONA CHA MOTO KWA AZAM

 
Michuano ya kombe la shirikisho Afrika imeendelea tena Jumapili kwa michezo kadhaa ,Azam fc wakicheza nyumbani Azam complex jijini Dar es salaam walifanikiwa kuwachapa Esperance ya Tunisia mabao 2-1.
Mchezaji wa Azam na Esperance wakichuana
Esperanace ndio walikuwa wa kwanza kupata bao lao dakika ya 33 kipindi cha kwanza kupitia kwa Haithem Jouini , baadaye Azam Fc wakasawazisha goli hilo na kuongeza bao lingine kupitia kwa wachezaji vijana wadogo Farid Mussa Malik na Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ waliofunga mabao hayo kipindi cha pili .

Farid Mussa ndiye aliyeanza kuifungia Azam dakika ya 68 baada ya kutanguliziwa pasi fupi na Singano Messi, na baadaye Ramadhan Singano akaifungia Azam bao pili na la ushindi dakika ya 70 kipindi cha pili.

Matokeo ya Mechi nyingine Ahli shendi ya Sudan imetoshana nguvu na Medeama ya Ghana 0-0, V Club imechapwa na Mokanda ya Congo bao 2-1, CF Mounana ya Gaboon imeifunga Enppi ya Misri bao 2-0.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii