MASAA 72 CHELSEA VS NORWICH

Klabu ya chelsea itakuwa nyumbani kumenyana na klabu ya Norwich City siku ya jumamosi tarehe 21Novemba 2015. 

Chelsea wanashika nafasi ya 16 katika msimamo wa ligi kuu Uingereza ikiwa mpaka sasa imejikusanyia jumla ya pointi 11 tu katika michezo 12 ambayo tayari wamecheza. 
Wachezaji wa chelsea wakitoka vichwa chini mara baada ya kufungwa moja ya mechi kwenye ligi kuu Uingereza
Wapinzani wao Norwich wapo juu wakishika nafasi ya 15 na pointi 12 katika michezo 12 ambayo tayari wameshiriki.
Wachezaji wa Norwich wakishangilia mara baada ya kupata goli katika moja ya mechi kwenye ligi kuu Uingereza

Chelsea ambao ni mabingwa watetezi, msimu huu wamejikuta wakiwa na wakati mgumu kupata pointi tatu kwa kila timu wanayokutana nayo kiasi cha kufanya kibarua cha kocha wao Jose Mourinho kuwa matatani. 

Katika mechi hiyo itakayoanza majira ya saa 11:00 jioni Chelsea pia wanatakiwa kurudisha imani kwa mashabiki wao watakao kuwa wamefurika uwanjani hapo Stamford Bridge kwa kutumia kila mbinu kuhakikisha wanapata ushindi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii