WALCOTT, STERLING WAIONGOZA ENGLAND USHINDI WA 2-0

 
Timu ya taifa ya Uingereza imerejesha matumaini mapya kwa mashabiki wa taifa hilo kutokana na hapo nyuma ambapo timu yao ya taifa ilikuwa ikiitwa tia maji tia maji kwani ushindi ulikuwa wa kubahatisha na sasa inaonekana ipo vizuri kwani kocha wao Roy Hodgson ameendelea kushinda mfululizo mechi tisa
Walcott akipachika bao safi wakati Uingereza ikiwa nyumbani uwanja wa Wembley dhidi ya Estonia mchezo wa kundi E michuano ya Euro-2016 hapo jana

Hodgson amesema kuwa alijitahidi kuwaandaa wachezaji wake wa timu ya taifa ya Uingereza vizuri ili kuhakikisha wanashinda mechi dhidi ya Estonia na anaamini mbegu hiyo itaendelea kufanya vizuri tena wakati huu wa michuano ya Euro 2016.
Uingereza imejinyakulia ushindi katika mechi zake zote tisa kwenye kundi E na kuendelea kujiweka vizuri katika michuano hiyo hata mara baada ya jana kushinda 2-0 dhidi ya Estonia. Magoli ya Uingereza yalifungwa na Theo Walcott na Raheem Sterling

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii