SERGIO ARGUERO NJE WIKI NANE

 
Majeraha ya siku 56 aliyoyapata mshambuliaji matata wa Manchester City ni pigo kubwa kwa timu hiyo inayoshiriki ligi kuu Uingereza na huku ikiwa mbioni kuutafuta ubingwa wa ligi hiyo kwani wanaongoza ligi wakiwa na alama 18 na Arguero huyo aliyeumia ndiye aliye funga magoli 5 katika mechi iliyopita.
Sergio Aguero is stretchered off during Argentina's World Cup qualifier against Ecuador
Sergio Aguero akitolewa nje wakati timu yake ya Argentina ikitafuta ushiriki wa kombe la dunia dhidi ya Ecuador
Sergio Aguero aliumia msuli wa mguu wakati akiichezea timu yake ya Taifa ya Argentina na huenda akawa nje ya uwanja kwa wiki nane.
Straika huyo wa klabu ya Manchester City alitolewa nje baada ya kuumia msuli unaounganisha sehemu ya paja na msuli wa chini ya goti (hamstring problem) wakati wa kipindi cha kwanza cha mchezo siku ya alhamisi ambapo Argentina walipigwa 2-0 dhidi ya Ecuador.
"Uchunguzi tulioufanya leo unaonesha Sergio Arguero aliumia misuli miwili inayounganisha paja na mguu,"  ni taarifa iliyotoka kwa chama cha soka cha Argentina siku ya Ijumaa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii