MOURINHO APIGWA FAINI

 
Meneja wa Klabu ya Chelsea Jose Mourinho amepigwa faini ya £ 50,000 na chama cha soka cha soka cha Uingereza FA.
 Katika adhabu hiyo Jose Mourinho pia amefungiwa mechi moja ambayo ni Chelsea dhidi ya Aston Villa.

 
 Adhabu hiyo imekuja baada ya meneja huyo wa Chelsea alikiri uvunjaji wa sheria za FA alipokuwa akiongea na vyombo vya habari mara baada ya mechi. 
Mourinho alishtakiwa kwa utovu wa nidhamu kufuatia mchezo dhidi ya Southampton uliochezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge Jumamosi Oktoba 3.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii