MESSI NA BABAKE WASHTAKIWA KWA WIZI
Jaji mmoja nchini
Uhispania ameagiza kwamba nyota wa timu ya Barcelona na Argentina Lionel
Messi, ni sharti ashtakiwe kwa mashtaka ya kuibia mamlaka ya ushuru
zaidi ya dola milioni 4.
Iwapo atapatikana na hatia atakabiliwa na kifungo cha miezi 22.
Jaji
huyo amesema kuwa Messi na babake Jorge, lazima wawasilishwe mahakamani
kwa madai kwamba walificha malipo yaliyotokana na haki zake za mauzo
huko Belize na Uruguay.
Jaji huyo pia alikataa ombi kutoka kwa kiongozi wa
mashtaka kwamba Jorge pekee ambaye alisimamia masuala ya fedha ya
mwanawe ndiye alipaswa kufunguliwa mashtaka.
Miaka miwili iliyopita wakati mashtaka hayo yalipofunguliwa, Messi na babake walilipa dola milioni tano kwa mamlaka ya ushuru.
Maoni
Chapisha Maoni